Karibu kwenye Lycamobile
Lycamobile ndio mwendeshaji mkubwa zaidi wa kimataifa wa mtandao wa simu za mkononi nao ni viongozi wa soko katika soko la simu za mkononi za malipo ya awali, ikiwa na wateja zaidi ya milioni 15 katika nchi 21 na mteja mpya akijiunga kila sekunde mbili. Ilianzishwa mwaka 2006 kwa ajili ya jamii za wataalamu barani Ulaya, nayo imekua haraka ikawa chapa inayojulikana sana duniani kwa kuwaunganisha wateja na wapendwa wao kuvuka bahari, mipaka na mitandao kwa bei ya chini zaidi iwezekanavyo.
Msambao mkubwa wa Lycamobile, umakinifu wake kwa huduma za wateja na mbinu bunifu ya kibiashara zimeiwezesha kuwapita washindani wake; imefanikiwa kuwafikia wakazi wa Ulaya kwa upana zaidi kuliko mwendesha mtandao mwingine yeyote. Kampuni hii inaendelea kuingia katika masoko mapya kwa ukawaida, hivi karibuni imeongeza Makedonia, na kuna mipango ya kuzindua nyinginezo mwaka huu.
Wateja milioni 15 na Idadi Bado Inaongezeka
Lycamobile huwaunganisha marafiki na familia kote duniani. Kwa sasa tunapatikana katika nchi 21 katika mabara makubwa matano nasi tunaandaa huduma ya kupiga simu, ujumbe na data za kitaifa na za kimataifa za ubora wa juu na bei ya chini. Sisi ndio mtandao wa kweli wa kimataifa ulio mkubwa zaidi duniani, tukiwawezesha watu kuwasiliana na marafiki na familia duniani kote bila kujali pale walipo
Chagua nchi yako ya Lycamobile kwenye orodha hapa chini